Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais huyo wa Uturuki amesema hayo kujibu uingiliaji wa moja kwa moja wa Misri katika masuala ya ndani ya Libya na kuongeza kuwa, vitendo vya Misri nchini Libya na uungaji mkono wake kwa jenerali muasi Khalifa Haftari anayeongoza kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya ni kinyume cha sheria.
Kabla ya hapo pia Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya ilikuwa imelaani vikali matamshi yaliyotolewa na Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri aliyetishia kuvamia kijeshi ardhi ya Libya.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Serikali ya Libya Khaled Al Mashri alisema kuwa vitisho vilivyotolewa na Abdel Fattah al Sisi havina maana yoyote kwa Walibya. Amesema katika ujumbe wake wa Twitter kwamba kutumia mamluki kama wawakilishi wa taifa la Libya kunaonesha jinsi siasa za Misri zilivyofilisika na kushindwa. Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Serikali ya Libya aidha amesema, Walibya wataendelea kujenga nchi ya kidemokrasia ya yenye mamlaka kamili.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya amesema kuwa, Tripoli inalaani vikali kikao kilichofanyika Cairo kwa jina la viongozi wa makabila ya Libya na kwamba Misri inapasa kuelewa kuwa maslahi yake yatalindwa kwa kushirikiana na serikali halali ya Libya. Fathi Bashagha aliongeza kuwa, GNA haitastahamili hatua yoyote ya kudunisha mamlaka ya Libya au kuteteresha serikali halali ya nchi hiyo.
342/